KIPIGO ch kuondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa kimeendelea kuzua tafrani kwenye klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam baada ya Zacharia Hans Poppe kujiuzulu jioni ya leo Makamu Mwenyekiti, Kaburu Nyange naye ameamua kubwa manyanga.
Habari ambazo Lenzi ya Michezo imezipata hivi jioni wakati Simba ikiwa kwenye mazoezi kwenye uwanja wa Itihad Mwananyamala zinasema kuwa Kaburu amemwandia barua Mwenyekiti Ismail Rage kumtaarifu uamuzi huo wa kujiuzulu wadhifa wake.
Hili litakuwa pigo la pili kwa Simba baada ya mchana wa leo Hans Pope kutangaza kujiuzulu.
Kuendelea kujiuzulu kwa viongozi kwenye klabu hii kongwe kunaweza kusababisha timu ikaendelea kufanya vibaya kwani hadi sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Yanga yenye pointi 42 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 36
Simba itashuka dimbani jumapili kucheza na Coastal Union yenye pointi 30 nyuma ya Simba
No comments:
Post a Comment