MIKAKATI YA KUENDELEZA
MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE
Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kwa
niaba ya kamati ya utendaji ya TWFA kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa
kutupa ridhaa ya kuongoza chama kwa kipindi cha miaka
minne.
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru
wadau wote wa mpira wa miguu kwa kutuwezesha kufika hapa tulipo. Napenda
niwashukuru wadau wote kwa ujumla wao na pia kuishukuru serikali kwa namna ya
pekee zaidi kwa mchango wake ,na mashirika na makampuni ambayo yamekuwa karibu
sana nasi NMB, SERENGETI, NSSF, PPF, na Bakheresa Group of
Companies.
Tunaamini kabisa kuwa vyombo vya habari ni washirika
wetu wakubwa katika kuendeleza mpira wa miguu wanawake. Napenda kuvishukuru
vyombo vyote vya habari hapa nchini na hata vile vya nje vilivyoweza kutoa
nafasi katika ujenzi wa mpira wa miguu wanawake.
Maendeleo ya mpira
Kutekeleza na kuendeleza mpango wa grassroot.
Kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania,Chama cha Mpira wa Miguu wanawake na vyama vya mikoa na wadau mbalimbali tutaendelea kuendeleza mradi wa mpira wa miguu kwa watoto wa kike na wa kiume Grassroot programme.(umri wa miaka 06-12).kwa mwaka 2013 mradi huu utatekelezwa katika mikoa mitano (5) mikoa hiyo ni Tanga, Pwani, Mwanza, Mtwara na Lindi. Mradi huu unaendeshwa kupitia shule za msingi.Kwa mwaka 2012 Mradi huu umeendeshwa katika mkoa wa Dar es Salaam na watoto wapatao 8766 (wasichana 4909 na wavulana 3857 ) na walimu 26 wameshirikishwa.
Mafunzo ,semina na makongamano
Kwa mwaka 2013
tunatengemea kuendesha mafunzo mbalimbali katika nyanja kuu nne za maendeleo ya
mpira wa miguu yaani Utawala na uongozi,Ualimu(Ukocha)
Uamuzi na utabibu katika mpira wa miguu .Katika mwaka mwaka 2013
mafunzo yatafanyika zaidi katika nyanja ya uongozi ili kuwajengea stadi za
uongozi viongozi wengi ambao wameingia madarakani katika chaguzi zilizofanyika
kwa mwaka 2012/2013.Mafunzo ya utawala na uongozi yatafanyika katika mikoa
nane:Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Mwanza,Musoma,Shinyanga,Kilimanjaro na
Tanga.Katika mafunzo hayo baadhi ya washiriki watateuliwa kutokana na uwezo wao
kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa na watahudhuria semina itakayo andaliwa kwa
kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania.
Mafunzo kwa walimu katika ngazi mbalimbali na uratibu wa utekelezaji wa mafunzo yaliyofanyika yatapewa kipau mbele.
Mafunzo kwa waamuzi yatalenga zaidi kuibua vipaji vya
watoto wa kike walioko mashuleni na wachezaji wanaomaliza/waliomaliza muda
wao.Mafunzo yatafanyika kwa awamu mbili katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Madaktari wa michezo ni
muhimu sana katika maendeleo ya mpira na afya za wachezaji kwa kushirikiana na
vyombo husika mafunzo kwa mwaka 2013 yatafanyika kwa awamu mbili na yatafanyika
katika mkoa wa Dar es Salaam.
Wanahabari wenye uweledi katika mpira wa miguu wa
wanawake ni chachu ya maendeleo ya mpira huo.Nafasi ya wanahabari ni kubwa
katika kuendeleza mpira wa miguu ili kuwajengea ujuzi zaidi kutakuwa na mafunzo
kwa wanahabari yatakayofanyika Dar es Salaam.
Uongozi na utawala bora
Maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake yanahitaji
viongozi bora na waliopewa ridhaa na vyombo husika.Chaguzi zimefanyika
katika mikoa 16 kati 25 ya mikoa ya Tanzania Bara.
Pia tunahimiza mikoa ambayo haijafanya uchaguzi ifanye chaguzi mapema.
Mikoa hiyo ni: Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Rukwa, Arusha, Geita,
Simiyu, Njombe, Katavi na Mbeya.
Katika chaguzi hizo kuna baadhi nafasi zote hazikujazwa ni matumaini yetu kuwa zitajazwa katika mikutano ijayo ya vyama husika.
Pia nichukue nafasi hii kuwahamasisha kina mama wengi
wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vya mikoa na taifa
pale uchaguzi utakapoitishwa.
Mashindano
Mashindano mbalimbali ndio moyo wa mpira wa miguu bila
mashindano hakuna anayeweza kutambua ubora na
kiwango chakena pia ni kipimo cha maendeleo.
Kutakuwa na mashindano mbalimbali katika ngazi
ya mikoa,taifa na kimataifa.
Mashindano hayo pia yatahusisha shule za
msingi na sekondari na vyuo mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyombo
husika kutakuwa na ufuatiliaji wa karibu wa michezo ya UMISSETA toka ngazi ya
mkoa hadi Taifa na kuwa na mpango endelevu wa kuwaendeleza wale wenye vipaji
ambao wamechaguliwa /wanaweza kuchaguliwa kwenye timu za taifa.
Ligi itachezwa katika ngazi za mikoa na baadaye kuunda
kombaini ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya taifa.
Kwa mwaka 2013 tunatengemea mikoa kuchezesha ligi
isiyopungua timu tano kwa mikoa 15 itakuwa na timu 10 na timu
itaruhusiwa kusajili wachezaji 25 kwa mwaka 2013 tunatengemea
watoto/wasichana 3750 kushiriki katika mpira wa miguu. Idadi hii
ukizidisha mara nne unapata jumla ya wachezaji 15,000.Endapo tutakuwa na benki
ya wachezaji hawa tutaweza kuunda timu bora za umri tofauti na zenye kiwango cha
juu.
Pia mikoa inahimizwa kuanzisha mashindano mbalimbali
yatakayoamsha ari kwa watoto wa kike na wasichana kushiriki katika mpira wa
miguu.
Uratibu wa mikoa
Wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na majukumu yao kama wajumbe watakuwa na jukumu la kuratibu shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu katika mikoa:Uratibu huo utakuwa kama ifuatavyo:
Rose
Kissiwa
|
M/ Mwenyekiti
|
Tabora, Dodoma, Rukwa, Kigoma,
Pwani
|
Amina
Karuma
|
Katibu
|
Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe,
Ruvuma
|
Zena Chande
|
Mjumbe
|
Dar es Salaam, Morogoro, Katavi, Shinyanga,
Mbeya
|
Triphonia
Temba
|
Mjumbe
|
Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga,
Singida
|
Sophia Charles
|
Mjumbe
|
Mara, Kagera, Simiyu, Geita,
Mwanza
|
Kwa mujibu wa katiba ya TWFA ibara ya
37 inatoa nafasi kwa kamati ya utendaji kuunda kamati ndogo za
kuendeleza mpira wa miguu wanawake kamati hizo ni kamati ya Fedha na
mipango,kamati ya Ufundi,kamati ya ngingine itakayoonekana inafaa.Kamati ya
utendaji kwa pamoja ilikubaliana kuunda kamati ya habari na
masoko.
Kamati ya Fedha na
Mipango
1.
Rose Kissiwa
- Mwenyekiti
2.
Evans
Aveva
3.
Sophia
Tigalyoma
4.
Sophia
Mukama
5.
Asha Baraka
Kamati ya
Ufundi
1.
Tryphonia Temba –
Mwenyekiti
2.
Florence
Ambonisye
3.
Miraji
Fundi
4.
Dr. Leonia
Kaijage
5.
Furaha
Francis
6.
Richard
Muhotoli
Kamati ya Habari na
Masoko
1.
Zena Chande –
Mwenyekiti
2.
Beatrice
Mgaya
3.
Mohamed
Mkangara
4.
Florian
Kaijage
5.
Somoe
Ng’itu
Masoko na Habari
Mpira wa miguu wanawake hauna udhamini na pia vyanzo rasmi vya kupata mapato.Kwa kupitia kamati ya habari na masoko ,tunaamini kutakuwa na mikakakti mbalimbali ya kuelimisha ,kuhamasisha wadau na watanzania wote kuwiwa na kujitoa kuendeleza mpira wa miguu .
Asanteni
Lina P.Kessy
Mwenyekiti Chama cha Mpira wa miguu
No comments:
Post a Comment