SHIRIKISHO la Soka nchini Libya, FLF
Jumatatu limemteua rais wa kwanza toka kuanzishwa kwa shirikisho hilo mwaka
1962.
Anouer al-Tachan
ndio jina lililoibuka kidedea katika uchaguzi huo ambao ulihudhuriwa na vilabu
mbalimbali nchini humo. Katika mfumo wa zamani shirikisho hilo
lilikuwa likimilikiwa na familia ya rais wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi
haswa watoto wa kiume wa rais huyo Saadi na Mohammed.
Mfumo mpya katika shirikisho hilo hivi
sasa una wajumbe wakuchaguliwa wapatao 12 ambao kazi yao kubwa itakuwa kuratibu
na kuweka mfumo mzuri wa uongozi katika kipindi cha mwaka mmoja
watakachotawala.
Ligi Kuu
nchini humo bado haijachezwa toka kuanguka utawala wa zamani mwaka 2011 kutokana
na harakati za kuhakikisha usalama unaimarika kwanza kabla ya kuanza.
No comments:
Post a Comment