KLABU ya Misr Lel Makasa ya nchini
Misri imewateua Hossam Hassan na pacha wake Ibrahim kuinoa timu hiyo msimu
huu.
Bodi ya klabu hiyo
ilikutana na kuamua kumfukuza aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Mohammed Abd El
Galel baada ya matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata katika
ligi.
Mwenyekiti wa Makasa Mohammed Abd El
Salaam alithibisha uteuzi wa Hossam na Ibrahim kuinoa klabu hiyo ambapo wataanza
kibaria hicho mapema wiki ijayo. Abd El Salaam alidai kuwa walianza
mazungumzo na ndugu hao wiki iliyopita na kuafikiana na mpango huo na anawaamini
wote wawili kama makocha wazuri na wanaweza kuikwamua timu hiyo na kuipeleka
mbali.
Mapacha hao ambao
ni wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Misri walikuwa wakifundisha klabu ya
Al Masry wakati maafa ya Port Saied yalipotokea mwaka 2011 na Zamalek katika
msimu wa mwaka 2010. Mbali
na timu hizo lakini pia waliisaidia timu ya taifa ya Misri kunyakuwa kombe la
Mataifa ya Afrika mwaka 1998 nchini Burnina Faso chini ya Mahmoud Al Gouhary
aliyekuwa akikinoa kikosi hicho wakati huo.
No comments:
Post a Comment