Aliyekuwa
kipa namba moja wa timu ya Yanga Yaw Berko amefanikiwa kusajiliwa
katika timu ya FC Lupopo ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.
Berko ambaye alitaka kuachwa na klabu yake aliondoka nchini hivi
karibuni kwenda kwenye majaribio na hatimaye amefanikiwa
kujiunga na klabu hiyo ambapo tayari klabu yake iliweka wazi kuwa asipofuzu majaribio hayo angetolewa kwa mkopo ili nafasi yake izibwe na
pacha wa Mbuyu, Kabange Twite.
Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa kuondoka kwa
beko haitaifanya timu hiyo kuyumba na wala haitafanya vibaya katika
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Alisema Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wenye uwezo mkuwa
hivyo ni matumaini yake kuwa Ally Mstafa ‘Barthez’ pamoja na Said Mohamed
wataziba vilivyo nafasi hiyo ya Berko.
“Ukiangalia hata katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Berko
hakucheza mechi nyingi lakini timu ilifanya vizuri hivyo kuondoka kwake
hakutotufanya tuharibu kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
“Tunaimani kubwa na makipa wetu waliyopo hivi sasa kuwa wana uwezo wa kuiongoza timu yetu kuhakikisha inafanya
vizuri mzunguko wa pili kama ilivyo kuwa kwa ule wa kwanza kwa sababu wa
uwezo na uzoefu na wamecheza ligi yetu kwa muda mrefu,” alisema
Mwalusako.
Berko alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty
Proffessional ya Ghana baada ya uwezo wake wa kulinda lango kumvutia
aliyekuwa kocha mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara
22 Kostadin Papic.
Katika hatua nyingine klabu hiyo leo inatarajia kuweka wazi wachezaji
wake iliyowaacha na wale iliyowaongeza kwa kwa ajili ya kuhakikisha
inatimza Lengo lake la kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ambao kwa
sasa unashikiliwa na Simba.
No comments:
Post a Comment