Kikosi cha Simba B |
Kikosi cha Serengeti boys |
Emily Mgeta akipambana na Bofu |
Mchezaji wa Serengeti boys Farid Shah akijaribu kumtoka Emlly Mgeta wa Simba B |
Kocha wa Simba B Suleman Matola akifuatailia mechi kwa makini |
TIMU ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 serengeti boys jana iliifunga Simba B bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Serengeti boys ambao wanajiandaa na mchezo wa raundi ya tatu wa kutafuta kufuzu fainali za vijana waliocheza kwa sana kuhahakisha wanapata bao na iliwachekua dakika 25 kupata bao kupitia kwa Farid Musa.
Simba B pia walicheza mchezo mzuri sana lakini umakini wa mabeki wa Serengeti boys uliwatibulia mipango yao ya kupata bao kwani kila wakiingia kwenye eneo la penalti au la goli tayari mabeki wanaondosha mpira.
Kikosi cha Serengeti boys kinachofundishwa na Jakob Michelsen kina kibarua kikubwa cha kuhakikisha wanaipeperusha vema bendera ya Tanzania kwa kufuzu kucheza fainali za vijana zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco, Machi mwakani.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Jakob Michelsen alisema anashukuru kiwango cha wachezaji kinaimarika ila anahitaji kupata michezo ya kimataifa ili aendelee kukipima kikosi hicho kabla ya kucheza mchezo wa raundi ya tatu.
"Nahitaji nipate michezo ya kimataifa maana michezi inayoikabili timu ni kutafuta kufuzu fainali za vijana hivyo kila timu inajiandaa vema", alisema Jakob.
Seleman Matola kocha wa Simba B alisema kuwa timu yake imefungwa lakini siyo kwamba kikosi chake kimecheza vibaya ila kimekutana na wachezaji wazuri maana wote wamecheza mchezo mzuri.
No comments:
Post a Comment