UONGOZI wa
klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga, amewatoa hofu mashabiki kuwa Nsa
Job anaendela vizuri baada ya
kugundulika kuwa hakuvunjika goti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
dhidi ya JKT Ruvu, kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam Jumapili
iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ahmed Aurora alisema kuwa wamefarijika
baada ya kupata taarifa za kitabibu toka kwa madaktari wa hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambapo amelazwa, zinaweka wazi kuwa Nsa Job hakuvunjika ingawa goti lake bali liligeuka lakini kwa sasa limerudishwa kwenye hali yake
ya kawaida na kufungwa bandeji gumu (P.O.P).
Pia alisema
kuwa katika mazingira hayo imekuwa ni faraja kubwa kwamba mshambuliaji huyo
anaweza kurejea uwanjani ndani ya muda mfupi tofauti walivyokuwa wanatarajia.
“Madaktari
wametudhibitishia kuwa hali yake inaendelea vizuri baada ya kugundulika kuwa
hakuvunjika goti ila liligeuka na kuwa nje ya njia yake ya kawaid hivyo imerudishwa na sasa anaendekea vizuri.
“Ni imani
yetu kubwa kwamba atarejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi
kutoka sasa kufuatia matibabu aliyopewa,” alisema Aurora.
Pamoja na
matokeo hayo mazuri ya mabao 3-0 kikosi chake iliyopata dhidi ya maafande wa
JKT Ruvu, mashambuliaji huyo alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumia
kufuatia kukosa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwenye uwanja huo hivyo
kupelekwa hospitali kwa usafiri wa kuunga unga.
Nsa Job
ambaye ni nyota wa zamani wa timu za Yanga na Villa Squad zote za jijini Dar es
Salaam aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Coastal Union
na JKT Ruvu ambapo mashabiki wengi wa soka walilaani kukosekana kwa ambulance
hiyo ambayo ni moja ya huduma kuhimu.
No comments:
Post a Comment