TIMU ya Azam FC imemfuta kazi kocha wake Boris Bunjak maarufu kama Boca
aliyechukua mikoba ya Mwingereza Stewart John Hall aliyetimuliwa kazi
mwezi tarehe 31/Julay/2012.
Boris
ambaye aliajiriwa kazi August 7 ya mwaka huu ametimuliwa kazi ikiwa ni
siku mbili zimepita baada ya Azam fc kupokea kichapo cha mabao 3-1 toka
kwa mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Simba mchezo uliofanyika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu
mwenyekiti wa Azam Said Mohamed Said alimsainisha Boris mkataba wa
miaka miwili huku kocha huyo akiondoka ndani ya viunga vya Chamazi
katika kipindi cha miezi mitatu.
Chini ya
Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika
nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame yakiwa
ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia katika historia
hiyo.
Wakati huu Boris akiondoka na akisakwa mrithi wake kwa sasa timu itakuwa chini ya fundi wa viungo Vivek Nagul na kocha msaidizi Kally Ongala.
Wakati huu Boris akiondoka na akisakwa mrithi wake kwa sasa timu itakuwa chini ya fundi wa viungo Vivek Nagul na kocha msaidizi Kally Ongala.
No comments:
Post a Comment