Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 7, 2012

YANGA YAZURU KIWANDA CHA BIA (TBL)

Mfanyakazi katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga, Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia zinavyopikwa jana Alhamisi, wakati timu hiyo yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga/Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
 



Wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na Benchi la Ufundi la timu hiyo, pamoja na baadhi ya viongozi wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) jana Alhamisi wakati timu hiyo ilipofanya ziara kiwandani hapo, Ilala jijini Dar es Salaam.
 
 
MABINGWA wa Kombe la Kagame Yanga, jana wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia nchini (TBL), kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam, ambacho kinaidhanmini klabu hiyo kupitia bia ya Kilmanjaro,.
Akiongea katika ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake iliamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinywaji mbali mbali, ikiwamo Kilimanjaro.

Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.

"Tunawaomba muendele na moyo huo  kwani sisi  Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora," alisema Sendeu.

Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo cha Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao, kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.

Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.

Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi, vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.

"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao. 

"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe
 

No comments:

Post a Comment