MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Bao la Yanga
lilifungwa katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza na Pius Buswita kwa
kichwa, akiunganisha wavuni mpira uliopigwa na Ibrahim ajib.
Sekunde
chache kabla ya bao hilo, Ruvu Shooting walikosa bao la wazi katika dakika ya
45 baada ya Abdulrahman Mussa kupiga shuti nje wakati kipa wa Yanga, Youthe
Rostand akiwa hayupo golini.
Ruvu
Shooting walikosa tena bao baada ya Issa Kanduru kushindwa kufunga katika
dakika ya 62 baada ya kufanikiwa kumpiga chenga kipa wa Yanga, Rostand kabla ya
kufunga beki Hassan Kessy kuokoa.
Kwa ushindi
huo, Yanga sasa imefikisha pointi 25 baada ya mechi 14, huku jahazi la Ruvu
Shooting likiendelea kuzama ikiwa na pointi 11 mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo
yenye timu 16.
Kwa pointi
hizo, Yanga imeitoa Mtibwa Sugar katika nafasi ya tatu, licha ya timu hizo kuwa
na pointi sawa, lakini mabingwa hao watetezi wana uwiano mzuri wa mabao.
Katika
mchezo mwingine wa ligi hiyo, Mwadui FC ambayo wiki iliyopita ilitoka sare na
Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, imetoka sare na Ndanda katika mchezo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
No comments:
Post a Comment