Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 29, 2014

MANCHESTER UNITED WAKIFANYA MAZOEZI KUJIWEKA SAWA DHIDI YA INTER MILAN, NA MAN CITY YAICHAPA AC MILAN BAO 5-1.

KLABU za Jiji la Machester, Mabingwa wa England Manchester City na Manchester United waliovuliwa Ubingwa na City, wanaongoza Makundi ya Mashindano ya International Champions Cup. Upo uwezekano kwao kukutana kwenye Fainali ya Mashindano haya hapo Agosti 4 ikiwa wataendeleza wimbi lao la ushindina hivyo kuhamisha uhondo wa Dabi ya Manchester huko Sun Life Stadium, Miami, Florida.Man United, ambao wako Kundi A, walianza kwa kuichapa AS Roma Bao 3-2 na Man City, walio Kundi B, kuishindilia AC Milan Bao 5-1, na matokeo hayo yamewafanya waongoze Makundi yao.
Kila Kundi lina Timu 4 na hivyo kila Timu kucheza Mechi 3 na Mechi zinazofuatia kwao ni Man United kucheza na Inter Milan kwenye Uwanja wa FedEx Field ndani ya Washington DC Jumatano Asubuhi na City kucheza na Liverpool Siku inayofuata huko Yankee Stadium, New York.
Kanuni za Mashindano haya ni tofauti kidogo kwani wakati Mshindi wa kila Mechi hupewa Pointi 3, ikitokea Timu kuwa Sare mpaka mwisho wa Dakika 90, Mikwaju ya Penati 5 hupigwa ili kupata Mshindi ambae hupewa Pointi 2 na aliefungwa Pointi 1.


Kocha wa United Louis van Gaal  akiwacheki vijana wake kwenye mazoezi.

 Shaw (katikati) na wenzake wakijifua tayari kwa mchezo wao na Inter Milan hapo kesho  Agosti 30

Juan Mata na Darren Fletcher wakisubiri maelekezo kutoka kwa mwalimu wao jana wakati wa Mazoezi

 Louis van Gaal na Chris Smalling kwenye Mkutano na Vyombo vya habari huko  Maryland

Jonny Evans, Danny Welbeck na Wilfried Zaha a wote wakijifua

 Evans, Will Keane na Michael Keane (kulia) wakijiweka sawa tayari kwa mtanange wao wa kesho na Inter Milan.

Wachezaji wa  Manchester United wakisikiliza nen kutoka kwa Kiongozi

Kipa David de Gea

 Juan Mata na Tom Cleverley

Wayne Rooney

Rooney na Evans wakisikilizia wakati wa mazoezi yao kujiweka sawa tayari kukwaana na Inter Milan Washington D.C. – FEDEXFIELD

RATIBA
Ijumaa Julai 25

Olympiacos CFP 3 AC Milan 0

Jumamosi Julai 26
Manchester United 3 vs AS Roma 2
Jumapili Julai 27
Real Madrid CF 1 vs Inter Milan 1 [Penati 2-3]
AC Milan 1 Manchester City 5
Jumatatu Julai 28
Liverpool 1vs  Olympiacos CFP 0

Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan [Washington D.C. – FEDEXFIELD]
05:15 Real Madrid CF v AS Roma [Dallas, Texas - COTTON BOWL]

Alhamisi Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool New York, NY - YANKEE STADIUM

Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma [Philadelphia, PA - LINCOLN FINANCIAL FIELD]

22:00 Olympiacos CFP v Manchester City [Minneapolis - TCF BANK STADIUM]
23:06 Manchester United v Real Madrid CF [Michigan Stadium - ANN ARBOR]

No comments:

Post a Comment