Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 21, 2018

SIMBA KUREJEA KILELENI KESHO?

SIMBA ya Dar es Salaam kesho inashuka kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya leo kuondolewa na Azam FC.
Azam FC jana iliitoa Simba kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.
Simba walitua salama kwa ndege mjini Bukoba na walifanya mazoezi kwenye uwanja huo wa Kaitaba wakijiandaa kwa pambano hilo linalotarajia kuwa kali.
Wekundu hao wa Msimbazi wanashuka dimbani  baada ya kuwachapa Singida United kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mganda Emmanuel Okwi baada ya juzi kutupia bao mbili peke yake wakati Simba ikiibuka na ushindi huo mnono, leo ataendelea kutegemewa na timu yake kutokana na makali yake.
Simba inashuka uwanjani leo ikiwa mkononi ina akiba ya pointi 29 baada ya kushuka dimbani mara 13, ikiwazidi pointi nne mabingwa watetezi Yanga, ambao jana waliifunga Ruvu Shooting 1-0.
Na sasa Wekundu wa Msimbazi kwa kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi, wamewasili mapema Bukoba kwa usafiri wa anga ili kufanya maandalizi mazuri.
Timu hiyo inacheza mchezo wake wa pili tangu kuwasili kwa kocha Mfaransa Pierre Lechantre aliyewasili wiki iliyopita na kuishuhudia timu hiyo ikiifunga Singida mabao 4-0.
Kocha huyo tayari ametambulishwa rasmi, lakini haijaelezwa ameingia mkataba wa miaka mingapi.
Ilielezwa kuwa kocha huyo Mfaransa ametua Simba kwa ajili ya programu maalumu ya vijana na ile ya timu ya wakubwa.
Lechantre ambaye ataanza kazi timu itakaporejea kutoka Bukoba, aliomba apewe angalau miezi minne ili Simba wafurahie matunda yake.

Kagera Sugar iko nafasi ya nne kutoka mkiani ikiwa na pointi zake 12 baada ya kushuka dimbani mara 13, hivyo ni timu dhaifu hadi sasa ukilinganisha na Simba.

No comments:

Post a Comment