Suarez akitokezea katika siku yake ya kwanza ya kusikiliza shauri lake la kupinga kufungiwa kwa miezi minne kufuatia kumng'ta Giorgio Chiellini |
Luis
Suarez ameondoka katika mahakama ya michezo duniani (Court of
Arbitration for Sport (CAS)) iliyoko mjini Lausanne baada ya masaa
matano ya usikilizwaji wa rufaa yake ya kupinga kufungiwa kwa miezi
minne ya kutokujishughulisha na na mchezo wa soka baada ya kumng'ata
Giorgio Chiellini katika kombe la dunia.
Suarez
aligomea kuongea lolote wakati akiondoka makao makao makuu ya CAS
nchini huko Uswiz mbali ya kusaini autographs na mashabiki wake
waliokuwa nje ya mahakama hiyo wakimsubiri.
Mshambuliaji
huyo wa Barcelona na timu yake ya wanasheria wana matumaini makubwa
kwamba adhabu dhidi yake yo iliyotolewa FIFA huenda ikapungua.
Endapo
hilo litatokea basi itakuwa ni njia kwa nyota huyo wa kimataifa wa
Uruguay mwenye umri wa miaka 27, kurejea tena katika soka baada ya
Agosti 25, na kuanza kuitumikia klabu yaje mpya katika ligi ya Hispania
dhidi ya Villarreal Agosti 31.
Encouragement: A young Barcelona fan wishes Suarez well and hopes to see him playing for his side soon
Wakili wa Suarez Alejandro Balbi, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini Uruguay amekaririwa akisema kuna nafasi finyu ya kubadilishwa kwa adhabu ya kusimama kwa michezo tisa ya kimataifa lakini huenda adhabu ya kusimama kwa miezi minne ikapunguzwa.
No comments:
Post a Comment