Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 19, 2018

MJUMBE WA KAMATI YA UENDAJI YA TFF AFUNGIWA MAISHA NA KAMATI YA MAADILI


MSIMAMIZI wa kituo cha Mtwara, Dustan Mkundi ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF amefungiwa maisha kujihusisha na soka na kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo.

Mkundi na wenzake wanne walipelekwa na sekretarieti TFF kwenye kamati ya Maadili viongozi kwa kosa la kughushi na udanganyifu wa mapato ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba na Ndanda FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Mtwara Desemba 30, 2017.

 Akizungumza leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Wakili Hamidu Mbwezeleni ambaye alisema kamati yake imewakuta na hatia Mkundi na kumfungia maisha kujihusisha na soka na Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano akafungiwa miaka mitano

Pia Mbwezeleni alisema Muhasibu msaidizi wa Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele hawakuwa na hatia.
“Sekretarieti iliondoa jina la Kahumbu kwenye mashtaka badala yake aligeuka kuwa shahidi katika kesi hiyo lakini Mkundi tulimkuta na hatia kwa sababu hesabu za mapato zilizopelekwa bodi ya ligi na TFF zimetofautiana,”
“Bodi ya ligi alipekeleka mapato ya sh milioni 37 lakini TFF aliwasilisha sh milioni 34 na timu za Ndanda na Simba zilipata mgao kutoka kwenye sh. milioni 37 hivyo udandanyifu ulifanyika katika mgao uliohusu TFF, BMT na TRA,” aliongeza Mbwezeleni.
Mbwezeleni alisema Mkundi aliwapelekea fomu nyingine Kahumbu na Kachele wamsainie kwa madai fomu za awali zilipotea na wawili hao waliisadia kamati kupata undani wa mapato lakini Mbano hakuwa tayari kukutana na kamati japo aliitwa mara tatu.
Aidha kamati hiyo imeitaka TFF kuhakikisha wanalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Kamati ya maadili iko chini ya Mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa.