Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 5, 2018

RATIBA YA HATUA YA 32 YA AZAM SPORTS FEDERATIONS CUP

YANGA na Azam FC zimeangukiwa kwa timu za daraja la pili katika hatua ya 32 ya Mashindano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambayo yanatarajiwa kuchezwa Januari 31 na Februari Mosi  mwaka huu.
Katika droo hiyo iliyozechezwa leo mubashara kwenye kituo cha Televisheni cha Azam Yanga watasafiri kwenda Mbeya kucheza na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine na Azam FC itamenyana na Shupavu FC ya Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri.
Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba itacheza nyumbani dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
KMC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Toto African ya Mwanza wakati Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya Mbao FC ya Mwanza na Majimaji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
Majimaji FC wataikaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Majimaji Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Kiluvya United ya Pwani wataikaribisha JKT Oljoro ya Arusha katika Uwanja wa Mabatini, Pwani na Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Pamba ya Mwanza wataikaribisha Stand United Shinyanga katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC ya Shinyanga wataikaribisha Dodoma FC ya Dodoma katika Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso ya Morogoro, Uwanja wa Sokoine Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC ya Geita katika Uwanja wa Kaitaba,  Bukoba, Kagera.
Droo hii imeshirikisha timu 32 ambapo timu nne ni za mabingwa wa mikoa, timu tatu  za Ligi Daraja la Pili, timu 12 za Ligi Daraja la Kwanza na 13 za Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment