Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 5, 2018

WAAMUZI WALIOCHEZESHA DODOMA FC DHIDI YA ALLIANCES WAFUNGIWA MIAKA 3

WAAMUZI waliochezesha mchezo wa Ligi daraja la kwanza dhidi ya Dodoma FC na Alliance Schools uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Desemba 30, 2017 wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu udhibiti wa waamuzi.
Akizungumza leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura alisema pamoja na kufungiwa waamuzi hao Kamati ya saa 72 imeomba suala la waamuzi hao ambao baadhi yao ni wa Ligi Kuu, kupitia TFF liwasilishwe kwenye chombo chenye dhamana ya kisheria ya rushwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.
“Waamuzi hao ni Andrew Shamba, Abdallah Mkomwa, Athuman Athuman na Omari Juma kwa kuchezesha mechi hiyo chini ya kiwango na Kamishna wa mechi hiyo Mackshem T. Nzunda kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo kwa usahihi,” alisema Wambura 
Pia Wambura alisema kamati imetupa malalamiko ya Alliance Schools kupinga uchezeshaji wa mwamuzi wa Andrew Shamba katika mchezo huo kwa vile hayakuwa na vielelezo wala kanuni za kuyathibitisha kwani suala la kutunza muda ni kazi ya mwamuzi.
Aidha mchezaji Shaban William wa Alliance Schools amesimamishwa, hadi suala lake la kumpiga mwamuzi litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF na timu hiyo imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa timu hiyo kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo.

Klabu ya Mufindi United, Mawenzi Market, Mkamba Rangers, Kitayosce zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja, kocha wa Green Warriors, Azish Kondo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 huku timu ya Nyanza FC ikishushwa madaraja mawili na kutozwa faini y ash 2,000,000

No comments:

Post a Comment