Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 2, 2018

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA FIFA


TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) utakaofanyika Februari 22, 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mkutano huo utashirikisha mataifa 19 ambao ni wanachama wa FIFA na Mwenyekiti wa mkutano akiwa anatarajiwa kuwa Rais wa FIFA Gianni Infantino
Akizungumza na wandishi wa habari jana Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia ni heshima kwa Tanzania na TFF kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa na kuwaomba wadau mbalimbali kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
“Tunamshukuru Mungu kupata fursa hii ya kuwa mwenyeji na ni faraja kubwa kwetu na nchini kupata nafasi hii kwani inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wasafi,” alisema Karia.
Karia alisema FIFA haiwezi kupeleka mkutano mkubwa kama huu bali kuna kitu wamekiona hivyo anashukuru uongozi wa nchi kwa namna wanavyoongoza kwa kufuata utawala bora
Pia Karia alisema miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa fedha za FIFA kwa ajili ya maendeleo ya soka, changamoto za usajili kwa njia ya mtandao Transfer Matching System (TMS).
Mataifa mengine yatakayoshiriki mkutano huo ni Algeria, Mali, Morocco, Burkinafaso, Angola, Niger, Bahrain, Palestina na Saud Arabia.

Mengine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Tunisia, Bermuda, Monserrat, St Lucia, Visiwa vya US Virgin, Maldives na  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment