Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 22, 2016

SAMATA AING'ARISHA GENK AKITUPIA BAO MBILI 


MTANZANIA Mbwana Samatta amezidi kuzikonga nyoyo za mashabiki wa klabu yake ya KRC Genk baada ya usiku huu kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Lokeren.

Samatta alipachika bao la kwanza la mechi hiyo ya ligi kuu nchini Ubelgiji katika dakika ya 34 na kuongeza la pili dakika nne tu baadae.

Genk walitawala kwa kiasi kikubwa mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Daknam Stadion na kupelekea kupata bao la tatu katika dakika ya 48 safari hii likifungwa na swahiba wa Samatta, mjamaica Leon Bailey.

Kwa ushindi huo Genk wamechupa hadi nafasi ya
 nne baada ya kufikisha alama saba katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Zulte-Waregem yenye pointi 10 wakifuatiwa na Anderlecht iliyojizolea pointi nane sawa na Sporting Charleroi.