Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 5, 2015

SIR ALEX FERGUSON KWENYE HISTORIA YA KIPEKEE YA WACHEZAJI WAKE 28 MAMENEJA

www.bukobasports.comSIR ALEX FERGUSON ni Lejendari aliewika na kuleta mafanikio makubwa katika Historia ya Manchester United lakini sasa matunda ya mafanikio yake yanatapakaa kila sehemu baada ya Wachezaji wake wasiopungua 28 kushika nyadhifa za Umeneja katika Klabu mbalimbali.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Man United ambae ataongezeka kwenye Listi hii ni Gary Neville ambae Jana alianuliwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Valencia inayocheza La Liga huko Spain.
PATA LISTI HIYO:
28. Mike Phelan
MENEJA: Norwich

Ndie alikuwa Msaidizi wa mwisho wa Sir Alex Ferguson wakati anastaafu kama Meneja wa Manchester United.
Sasa ni Msaidizi Hull City.
27. Gabriel Heinze
MENEJA: Godoy Cruz


Beki wa zamani wa Argentine na Mwezi Juni alichukua wadhifa wa Klabu ya Nchini kwao na kutimuliwa Mwezi Septemba.
26. Viv Anderson
MENEJA: Barnsley

Alidumu Msimu mmoja tu kama Meneja-Mchezaji wa Barnsley na kisha kwenda kumsaidia Nahodha wa zamani wa Man United, Bryan Robson, ambae alikuwa Meneja wa Middlesbrough na kisha kuachana kabisa na Umeneja na sasa ni Mchambuzi mahiri.
25. Neil Webb
MENEJA: Weymouth, Reading Town

Ni Kiungo wa zamani wa Man United alietwaa FA Cup Mwaka 1990. Baada ya kustaafu Soka aliongoza Klabu kadhaa zilizokuwa nje ya Ligi lakini sasa ni Mchambuzi.
24. Pat McGibbon
MENEJA: Lurgan Celtic, Newry


Hakucheza mara kwa mara Man United akikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara mpaka alipostaafu na kuongoza Klabu kadhaa za kwao Ireland ikiwa moja ni Mji wa kwao, Lurgan Celtic.
23. Paul Parker
MENEJA: Chelmsford, Welling


Alikuwa Fulbeki mahiri kwenye Kikosi cha Ferguson kilichotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza na kisha kuwa Meneja wa Klabu zisizo kwenye Ligi bila mafanikio.
22. Clayton Blackmore
MENEJA: Bangor, Porthmadog

Alifundisha Klabu kadhaa za kwao Wales.
21. Teddy Sheringham
MENEJA: Stevenage

Kazi yake ya kwanza ya Umeneja ni kwenye Timu ya Ligi 2, Stevenage, lakini mambo si murua huko na hii ilikuja baada ya kuwa Kocha wa Mastraika huko West Ham.
20. Peter Davenport
MENEJA:
Macclesfield, Bangor, Colwyn Bay, Southport

Alikuwa na Ferguson katika Misimu yake Miwili ya kwanza na kisha kuingia Umeneja kwenye Klabu kadhaa lakini tangu 2010 hafanyi kazi.
19. Frank Stapleton
MENEJA:
Bradford, New England Revolution

Alikuwa Meneja-Mchezaji wa Bradford City Mwaka 1994 na kisha huko Marekani kwenye Klabu ya MLS New England Revolution alikodumu Miezi 9 tu. Sasa ni Msaidizi wa Ray Wilkins kwenye Timu ya Taifa ya Jordan.
18. Simon Davies
MENEJA:
Chester
Huyu ni mmoja wa ile Grupu ya Wachezaji maarufu ‘Class of 92’, iliyokuwa na kina Beckham, Giggs, Butt, Neville, lakini aliuzwa na Ferguson Mwaka 1997 na kisha kujiunga kama mmoja wa Makocha wa Chester.
17. Ryan Giggs
MENEJA:
Manchester United
Huyu ni Lejendari wa Man United ambae mwishoni mwa Msimu wa 2013/14, alipotimuliwa David Moyes, alikaimu kama Meneja.
Sasa ni Meneja Msaidizi wa Man United chini ya Louis van Gaal.
16. Andrei Kanchelskis
MENEJA:
Torpedo-Zil Moscow, Ufa, Jurmala
Huyu alikuwa Winga hatari na alipostaafu aliongoza Klabu kadhaa za kwao Urusi.

15. Chris Casper
MENEJA:
Bury
Ni Beki aliestaafu akiwa na Miaka 23 tu baada ya kuumia vibaya na kujikita kwenye Ukocha.

Sasa anashughulika na Klabu kadhaa kusaidia kujenda Vyuo vyao vya Soka.
14. Chris Turner
MENEJA:
Leyton Orient, Hartlepool, Sheffield Wednesday, Stockport

Ni Kipa aliedunmu na Ferguson kwa Miaka Miwili na kisha kuingia Ukocha na Umeneja.

13. Michael Appleton
MENEJA:
Portsmouth, Blackpool, Blackburn, Oxford United

Alicheza Mechi 2 tu za Man United chini ya Ferguson na kisha kujiunga na Preston.
Alistaafu Soka mapema baada ya kuumia Goti.

12. Roy Keane
MENEJA:
Sunderland, Ipswich

Baada ya kustaafu Soka, Nahodha huyu wa zamani wa Man United alitua Sunderland kama Meneja na kuipa Ubingwa wa Daraja la Championhip Mwaka 2007 na kuipandisha Ligi Kuu England.
Lakini hakufanikiwa na Sunderland na kuondoka na kisha kuiongoza Ipswich ambako hali ilibaki vilevile.

11. Paul Ince
MENEJA:
Macclesfield, Milton Keynes Dons, Blackburn, Notts County, Blackpool
Alikuwa Kiungo mahiri wa Man United ambae ameweza kuwa Meneja wa Klabu kadhaa huko England.

10. Henning Berg
MENEJA:
Lyn, Lillestrom, Blackburn, Legia Warsaw

Ni Beki wa Man United kutoka Norway ambae alipostaafu aliingia kwenye Ukocha. 


9. Mark Robins
MENEJA:
Rotherham, Barnsley, Coventry, Huddersfield, Scunthorpe
Alistaafu Mwaka 2005 na kuwa Meneja wa Klabu 5.
Sasa ni Meneja wa Scunthorpe ambayo ipo Ligi 1.

8. Henrik Larsson
MENEJA:
Landskrona, Falkenbergs, Helsingborgs

Ni Lejendari wa Sweden na Klabu ya Celtic aliecheza kwa Mkopo Man United Mwaka 2007.
Miaka Mitatu baadae akaanza Umeneja kwenye Klabu za kwao Sweden.

7. Ole Gunnar Solskjaer
MENEJA:
Molde, Cardiff

Baada ya kustaafu Soka alipewa jukumu la kufundisha Vijana wa Man United na baadae akateuliwa Meneja wa Klabu ya kwao Norway, Molde, ambayo aliiongoza kutwaa Ubingwa wa Norway mara 3.
Kisha akatua Cardiff City lakini akaondolewa na sasa yupo tena Molde.

6. Bryan Robson
MENEJA:
Middlesbrough, Bradford, West Brom, Sheffield United, Thailand

Alikuwa Nahodha mahiri wa Man United na England na alipostaafu alikuwa Meneja wa Middlesbrough.
Hivi sasa ni mmoja wa Mabalozi wa Man United.

5. Darren Ferguson
MENEJA:
Peterborough, Preston, Doncaster

Ni Mtoto wa Ferguson aliefanikiwa kuipandisha Daraja mara 2 alipokuwa Meneja wa Peterborough na sasa yupo Klabu ya Ligi 1 Doncaster.

4. Gordon Strachan
MENEJA:
Coventry, Southampton, Celtic, Middlesbrough, Scotland
Kama Meneja, alipata mafanikio mazuri na Coventry na kuziongoza Klabu kadhaa.
Hivi sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Scotland.

3. Steve Bruce
MENEJA:
Sheffield United, Huddersfield, Wigan, Crystal Palace, Birmingham, Sunderland, Hull

Ni Sentahafu mahiri wa Man United chini ya Ferguson ambae alipostaafu ameziongoza Klabu maarufu kadhaa za England kama Meneja.

Hivi sasa yupo Hull City ambayo ipo Daraja la Championship.
2. Mark Hughes
MENEJA:
Wales, Blackburn, Manchester City, Fulham, QPR, Stoke
Sasa ni Meneja wa Stoke City ambae amewahi kuziongoza Klabu nyingine kadhaa ikiwemo Timu ya Taifa ya Wales.

1. Laurent Blanc
MENEJA:
Bordeaux, France, Paris Saint-Germain
Huyu ni Kepteni wa France iliyotwaa Kombe la Dunia ambae aliwahi kucheza chini ya Ferguson.
Ana mafanikio makubwa kama Meneja wa Klabu za kwao France ambako pia aliwahi kuwa Meneja wa Timu ya Taifa.
Alitwaa Ubingwa wa France akiwa na Bourdeaux na sasa yupo PSG ambako tayari ashatwaa Ubingwa mara 3, French Cup 1 na Kombe la Ligi mara 3.