Uchaguzi wa Kamati ya Uongozi ya Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania Bara utafanyika Oktoba 15, 2017 Dar es Salaam.
Fomu kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa Agosti 17, 2017
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mwisho wa kuchukua
na kurudisha fomu kwa wagombea ni saa 10.00 jioni Agosti 23, mwaka huu.
Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe
watatu kuwakilisha klabu za Ligi (PL), Wajumbe wawili wa kuwakilisha klabu za
Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha klabu za Ligi
Daraja la Pili (SDL).
Ada ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni Sh
200,000 (Shilingi lakini mbili) wakati nafasi nyingine zilizobaki ni Sh 100,000
(Shilingi laki moja).
Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF
toleo la 2013.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu
ni marais au wenyeviti wa klabu husika.
Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
No comments:
Post a Comment