Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), limepokea malalamiko kutoka baadhi ya timu na vituo vya kuibua na kukuza
vipaji vya soka zikidai fidia baada ya wachezaji wao kusajiliwa na klabu
nyingine msimu wa 2017/18.
Jana Agosti 14, 2017 ilikuwa siku ya mwisho kwa timu na vituo
vya kuibua na kukuza vipaji kuwasilisha malalamiko yao TFF kuhusu fidia za
mafunzo; ada ya usajili; ada za maendeleo na kuvunjwa kwa mikataba kutoka
katika timu walizochezea hadi msimu uliopita.
Alliance ya Mwanza imelalamikia Pamba pia ya Mwanza kuhusu
mchezaji Juma Nyangi ambako madai hayo yamekwenda mbali zaidi yakisema kuwa
mchezaji husika amebadili jina kwa lengo la kudanganya.
Kwa upande wake, African Lyon imeondokewa na wachezaji 19 na
inadai fidia katika timu, wachezaji kwenye mabano za Majimaji (Saleh Malande);
Lipuli (Hamad Manzi, Lambele Reuben na Mussa Nampoka); Young Africans (Rostand
Youthe Jehu); Tusker FC (Abdul Hilal) na Ndanda kwa wachezaji Hamad Tajiri na
Baraka Majogoo.
Madai mengine ni dhidi ya Coastal Union kwa wachezaji Baraka Jaffary,
Omary Salum, Raizen Hafidh na Fred Lewis huku madai mengine ni kwa Kagera Sugar
kwa wachezaji Omar Abdallah, Abdallah Mguhi na Vicent Ludovic na Alhaji Zege .
Madai mengine ni dhidi ya timu ya Kinondoni Municipality Council
(KMC) ambayo imewasajili Halfan Twenye, Yussuf Abdul na Rehani Kibingu wakati
Singida United inalalamikiwa kumsajili Miraji Adam ilihali Njombe Mji inadaiwa
fidia kwa kumsajili mchezaji Salum Juma.
Malalamiko mengine ni ya Kisa Academy ya Kinondoni, Dar es
Salaam dhidi ya timu za Mbeya City (Idd Seleman); Majimaji (Jafar Mohammed);
Mbao (Ally Rashid); Stand United (Said Mbati) na Friends Rangers (Hassan
Abubakar).
Madai mengine dhidi ya timu za Coastal Union (Abubakar
Nyakarungi na Ahmed George); The Mighty Elephant (Maliki Hamad); Kagera Sugar
(Hussein Idd) na Azam FC (Omary Maunda).
Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji
kinatarajiwa kuketi Jumapili kupitisha usajili lakini kabla kitapitia
malalamiko hayo na kuchukua uamuzi.
No comments:
Post a Comment