Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 4, 2017

OBREY CHIRWA HURU KUIVAA MTIBWA KESHOImage result for OBREY CHIRWA
MSHAMBULIAJI wa Yanga Obrey Chirwa yuko huru kuchezea  kesho katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kufutiwa kadi moja ya njano
Chirwa amefutiwa kadi moja ya njano na kusababisha kuondoka kwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema kadi hiyo imefutwa baada ya kubainika mchezaji huyo alionyeshwa kimakosa.
“Kadi ya Chirwa imefutwa kufuatia Yanga kuwasilisha malalamiko dhidi ya mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera na Bodi imejiridhisha kwamba mwamuzi huyo alipitiwa, hivyo kuifuta kadi hiyo na sasa yuko huru kuichezea timu yake katika mchezo ujao,”amesema
Chirwa alionyeshwa kadi mbili za njano za utata ndani ya dakika mbili na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 katika mchezo ambao Yanga ilishinda 2-0.
Alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 44 baada ya kuifungia Yanga bao safi ambalo lingekuwa la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Hassan Kessy, lakini mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera akalikataa na kumuonyesha kadi ya njano.
Kadi ya pili njano alionyeshwa dakika ya 45 baada ya kuudunda mpira chini na kutolewa kwa kadi nyekundu.
Yanga imeondoka leo Alfajiri Dar e Salaam kuelekea Morogoro tayari kwa mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar.