Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 7, 2024

ZENA CHANDE, SOMOE NG'ITU WACHUKUA FOMU KUGOMBEA TWFA

Zena Chande

Somoe Ng'itu


WANAHABARI wakonge Zena Chande na Somoe Ng’itu wamechukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi tofauti kwenye Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) unaotarajiwa kufanyika Septemba 14, mkoani Kilimanjaro.

Somoe ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa TWFA amechukua fomu kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho wakati Zena ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kutoka TWFA anawania kutetea nafasi yake.

Zena ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari wa gazeti la HabariLEO ni mzoefu katika nafasi mbalimbali za soka ikiwemo ikiwemo nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kadhalika ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake ya TFF hadi sasa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA mkoa wa Dar es Salaam.

Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Tuzo ya TFF kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 na ni Kamishna wa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi sasa.

Kuhusu Somoe pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe na Kamishna wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwenyekiti wa TWFA Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake ya TFF.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamati ya uchaguzi huyo, Makamu Mwenyekiti Benjamin Kalume alisema wagombea walianza kuchukua fomu leo na mwisho ni Jumapili.

Pia alisema nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Mwakilishi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji nafasi mbili.

“Mchujo utaanza Jumatatu Agosti 12 hadi 14 mwaka huu, majina yatachapishwa Agosti 15-16 na kuweka pingamizi na kupokelewa ni Agosti 16-19,” alisema Kalume.

Aidha alisema kamati itapitia mapingamizi Agosti 20-22 na majina yatatangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo Agosti 23 na 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment