“Ni muhimu sana kwa kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huo ni wito kwa viongozi wa soka hapa Tanzania na wadau wote wa michezo kuweka nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni,
“Ni muhimu kama taifa kuwekeza kwa vijana kuwaweka mazingira na miundombinu ya kutosha kabisa ili kuweza kuinua vipaji vyao vya soka na ndio staili inayotumiwa na mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Barnes.
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya
kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana
chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu
nchini.
Katika siku yake ya tatu (leo) nchini
gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za
Tanzania, Uganda na Kenya ambao watapambana vikali kuwania kombe la
Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool
nchini Uingereza.Barnes amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na kuwa tegemeo katika nchini yao.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
“Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na
timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya
kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth
Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kwamba takribani timu 32
zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya kutafuta mwakilishi wa
Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na timu mbili kutoka
Uganda na Kenya.Mramba alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana wadogo.
Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia.
“Hii ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana ni mastaa wa taifa wa baadaye,” alisema.
Aidha, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake.
Aliongeza kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania.
Gwiji hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na wanahabari
(hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na miundombinu
ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka nchini.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu
ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto
chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati
wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool,
John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya
miaka 15.
Pichani
juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi
kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata
fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la
Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha
miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo
katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Timu ya
taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho
baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya
Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth
Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja na
baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata
nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.
No comments:
Post a Comment