VINARA wa
Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameshindwa kuondoka na pointi tatu
baada ya kulazimishwa sare kufungana mabao 2-2 na Mbeya City `Koma Kumwanya’katika
mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wenyeji
Simba walionekana kuzidiwa katika kipindi cha kwanza baada ya Mbeya City kupata
bao la kuongoza katika dakika ya 37 lililofungwa na Ditram Nchimbi kufuatia
pasi ya Kenny Ally.
Simba
walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 65 mfungaji akiwa ni Ibrahim
Ajibu, baada ya kupiga mpira wa adhabu uliojaa wavuni moja kwa moja.
Mbeya City
waliongoza tena baada ya kupata bao la pili katika dakika ya 78 lililofungwa na
Kenny Ally baada ya kupata pasi kutoka kwa Nchimbi.
Dakika nne
kabla ya mchezo kumalizika, Simba walipata bao la kusawazisha lililofungwa kwa
penalti na Kichuya baada ya Mohamed Hussein kuangushwakatika eneo la hatari.
Simba
ilifanya shambulio la nguvu katika dakika ya 12 na Kichuya alikosa bao la wazi
baada ya kichwa alichopiga kudakwa na kipa wa Mbeya City, Own Chaima.
Ajibu nusufa
afunge katika dakika ya 40, lakini lilimbabatiza kipa wa Mbeya City na kutoka
nje.
Timu hizo
zilikwenda mapumziko Mbeya City ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kwa matokeo
hayo, Simba imefikisha pointi 55 na kuwa mbele kwa pointi tatu dhidi ya
mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wenye pointi 52, ambao leo
wanacheza na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Simba wiki
iliyopita iliifunga Yanga mabao 2-1 na kutarajiwa kuonesha makali zaidi katika
mchezo huo wa jana dhidi ya Mbeya City, ambayo mwendo wake sio mzuri katika
ligi hiyo.
Vikosi vilikuwa, Simba:
Daniel
Agyei, Hamas Juma, Mohamed Hussein, Abdi banda, James Kotei, Jonas Mkude,
Mzamiru Yasini, Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo, Said Ndemla na Shiza Kichuya.
Mbeya City:
Own Chaina,
John Kabanda, Majaliwa Shabani, Tumba Sued, Rajabu Zahiri, Kenny Ally, Sankani
Mkandawile, Raphael Daud, Ditram Nchimbi, Mrisho Ngasa na Rafael Brayson.
No comments:
Post a Comment