Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 5, 2017

YANGA YABANWA KAMA SIMBA



MABINGWA watetezi Yanga leo Imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sare hiyo inayokuja siku moja baada ya mahasimu wao, Simba kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuifanya Yanga kushindwa kupanda kileleni.
Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha pointi 53 baada ya kucheza mechi 24 ikizidiwa pointi mbili na Simba yenye pointi 55 katika michezo 24 iliyocheza na Mtibwa inaendela kubaki katika nafasi yake ya tano ikiwa na pointi 34.
Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva alishindwa kuifungia Yanga dakika ya 35 baada ya kupiga penalti ambayo ilipaa juu, kufuatia Ally Lundenga wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira kwenye eneo la penalti.
Adhabu hiyo ilitokana na mpira uliorushwa na beki Oscar Joshua na katika kuwania mpira Lundenga  wa Mtibwa Sugar na Obrey Chirwa ndipo mchezaji huyo wa Mtibwa akaunawa mpira kwa bahati mbaya.
Kikosi cha Mtibwa Sugar ni Said Mohammed, Shaaban Nditi, Haroun Chanongo/Kevin Friday dk75, Stahmil Mbonde/Hussein Javu dk 83, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Ally Lundenga, Salim Abdallah, Mohammed Issa, Jaffar Ally, Ally Shomary na Ally Makarani.
Yanga ni Deogratias Munishi ‘Dida’, Hassan Hamisi, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Kevin Yondan/Said Juma ‘Makapu’ dk 70, Simon Msuva, Justine Zulu, Obrey Chirwa, Malimi Busungu/Juma Mahadhi dk 31 na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk 60.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wenyeji African Lyon waliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC.
African Lyon inapanda hadi nafasi ya 12 ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 25 na Mwadui FC inaendelea kubaki kwenye nafasi yake ya sita na pointi 31.

No comments:

Post a Comment