Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 17, 2017

TFF YAMLILIA GEOFREY NA MBAGASHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa salamu za pole kufuatia vifo vya wachezaji wawili walioaga dunia usiku wa kuamkia leo .
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas wamepokea kwa masikitiko taarifa za kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Godfrey Bonny ambaye alikuwa anaumwa na mchezaji wa Green Warriors Julias Mbaga.
“Tumepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bonny kwani ni mchezaji ambaye ameacha alama kwenye soka letu na TFF inashiriki kikamilifu kwenye msiba huu kupitia uongozi wa Chama cha soka Mkoa wa Mbeya,” alisema Lucas
Godfrey ambaye pamoja na kuichezea Yanga pia amewahi kucheza Taifa Stars mara kadhaa chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo.
Kabla ya kujiunga Yanga Geofrey ambaye alizaliwa 1980 alikuwa askari wa jeshi la Magereza na alikuwa anachezea timu ya Tanzania Prisons na amefariki akiwa nyumbani kwao Mbeya baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Julias Mbaga ambaye alikuwa anachezea timu ya Green Warriors  ya daraja la pili yeye alikuwa amelazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali Dodoma wakitokea Shinyanga kucheza na Bulyankulu
Mwili wake upo hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo na taratibu za mazishi zinafanywa na familia yake kwa kushirikiana na timu ya Green Warriors