MASHABIKI wa Yanga wameonywa kutoingia na mabango uwanjani yenye kukashifu serikali wakati wa mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ngaya utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Onyo hili limetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata taarifa kuwa mashabiki wa Yanga wamepanga kuingia na mabango yenye maandishi kukashifu viongozi wa serikali na uongozi wa TFF.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema ni marufuku kuonyesha mabango yenye kukashiru na kutukana viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa TFF na endapo mtu atakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa.
“Tunawaonya mashabiki wasithubutu kuingia na mabango kwani atakakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashtaka kwenye mahakamani,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema taarifa za uhakika ambazo wamezipata zinadai mashabiki hao wamepanga kuingia na mabango hayo kwenye mchezo wa kesho (leo) na ule wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Februari 25.
Lucas amesema kitendo chochote cha kukaidi amri hiyo ni kinyume cha sheria kwani TFF ina wajibu wa kusimamia usalama kwenye viwanja vya soka.
Pia amewakumbusha kuwa usalama umeimarishwa kwani pamoja na askari wa kulinda usalama kuna kamera ambazo zina uwezo wa kuonyesha kila mtu uwanjani na anachofanya hivyo inakuwa rahisi kumfuatilia na kumkamata.
Yanga inashuka
dimbani leo kucheza na Ngaya ya Comoro, ukiwa ni mchezo wa marudiano wa raundi
ya awali wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga imepewa nafasi
kubwa ya kushinda na kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza kushinda 5-1
No comments:
Post a Comment