MABINGWA
wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1 katika
mechi ya kujiandaa na msimu mpya iliyopigwa Uwanja wa Taifa jana.
Yanga
inayonolewa na Erie Brandts ilianza kuonesha umahiri wake kwenye dakika ya 26
baada ya Said Bahanuzi kumalizia krosi ya Jerryson Tegete hivyo kuwanyanya
mashabiki wao katika viti.
Yanga
yenye Makao Makuu yake Jangwani jijini Dar es Salaam iliendelea kulisakama
lango la Mtibwa, ila uhodari wa Kipa Hussen Sharifu wa Mtibwa, ulionekana baada
ya kuokoa michomo mbalimbali iliyopigwa na washambuliaji wa miamba hiyo ya
Bara.
Hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lakini cha pili
kilipoanza tu, Mtibwa walionekana kuamka ambapo dakika ya 57 walipata bao kwa
njia ya penalti iliyofungwa na Shabani Kisiga baada ya Rajab Zahir kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari.
Mara
baada ya bao hilo, Mtibwa waliliandama lango la Yanga mara kwa mara ambapo
dakika ya 60, Ally Mohammed alishindwa kuifungia timu yake baada ya kupiga
shuti hafifu lilookolewa na Deo Munishi.
Ndoto
za Mtibwa kuibuka kidedea kwenye mchezo huo zilizimwa dakika ya 81 baada Tegete
kuzamisha wavuni penalti waliyoipata kufuatia Salvatory Ntebe kumwangusha
mfungaji huyo kwenye eneo la hatari.
Uzembe
wa Kipa, Saidi Mohammed aliyeingia kipindi cha pili, uliigharimu Mtibwa dakika
ya 87 baada ya Hussein Javu kumpiga chenga na kutikisa nyavu hizo kirahisi.
Hadi
mwamuzi anamaliza mchezo huo, Yanga ilifanikiwa kushinda 3-1 licha ya Mtibwa
kuonesha kandanda safi kipindi cha pili.
Yanga
iliwakilishwa na Deo Munishi/Ally Mustaph, Juma Abdul, Oscar Joshua,
Issa Ngao, Nadir Haroub/Rajab Zahir, Athuman Iddi/ David Luhende, Said
Bahanuz/Abdallah Mguli, Salum Telela, Shaban Kondo/Husein Javu, Jeryson Tegete
na Haruna Niyonzima
Mtibwa:
Hussen Sharifu/Said Mohammed, Hassan Ramadhan, Paul Ngalema, Ally
Ramadhani/Dikson Daudi, Salvator Ntebe, Salim Mbonde, Ally Shomary, Masud
Ally/Awadh Juma, Abdallah Juma/Stanley Minzir, Shabani Kisiga na Ally Mohammed.
No comments:
Post a Comment