Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 28, 2014

BAADA YA KUSAJILIWA NA EVERTON ETO'O AFUNGUKA! ADAI HANA BIFU NA JOSE MOURINHO WA CHELSEA.

Samuel Eto'o ametupilia mbali madai kuwa ana bifu na Jose Mourinho wakati timu yake mpya Everton ikijitayarisha kuikabili Klabu yake ya zamani Chelsea hapo Jumamosi.
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroon, na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho walikuwa pamoja huko Inter Milan na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI pamoja na akaja England Mwaka mmoja uliopita kuungana na Mourinho huko Chelsea.
Lakini uhusiano wa Eto’o na Mourinho ulipata msukosuko pale Mreno huyo aliponaswa kwenye Kamera bila kujijua akidhihaki Umri wa Eto’o na kudai ni Mzee kupita Miaka inayodaiwa anayo.
Mara baada ya tukio hilo Eto’o, mwenye Miaka 33, alifunga Bao akiichezea Chelsea na kwenda kushangilia mithili ya Mzee akishika Kibendera cha Kona kama Mkongojo huku akijishika Kiuno ili kumdhihaki Mourinho.
Akiongea na Wanahabari mara tu baada ya kutambulishwa kama Mchezaji mpya, Eto’o alipuuza madai hayo ya kuwa na bifu na Mourinho na badala yake kusema anamshukuru Mourinho kwa kumleta Ligi Kuu England.
Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez amedokeza kuwa huenda Mkongwe huyo wa Cameroon akaivaa Chelsea Jumamosi wakati watakapopambana Goodison Park katika Mechi ya Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment