Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 25, 2015

WAYNE ROONEY, MARTIAL WAUNGANA NA WENZAO KWENYE MAZOEZI KUCHEZA MCHEZO WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO DHIDI YA PSV

Kepteni Wayne Rooney Mazoezini sasa baada ya kupona majeraha yake na sasa amejumuika na wenzake kwenye mazoezi kujiandaa vyema na Kipute cha UEFA Champions League dhidi ya PSV jumatano.
Manchester United wanahitaji ushindi kwenye Mechi yao hii na PSV Eindhoven Uwanjani Old Trafford ili wafuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi moja mkononi.
Lakini PSV, inayoongozwa na Kocha Phillip Cocu, ambae alikuwa Mchezaji chini ya Meneja wa Man United Louis van Gaal huko Barcelona, iliifunga Man United 2-1 katika Mechi ya kwanza huko Amsterdam.
PSV wanaingia Mechi hii ya Old Trafford wakiwa hawajashinda hata Mechi moja ya Kundi B la UCL ya Ugenini baada ya kufungwa na CSKA Moscow na Wolfsburg.
Kwenye Ligi yao huko Uholanzi, PSV wako Nafasi ya Pili baada ya Juzi Jumamosi kuongoza 1-0 walipocheza na Willem II na kutoka Sare 2-2.
Wayne Rooney na Meneja Van Gaal wakati wa Mazoezi wakiteta jamboWayne Rooney na Juan Mata wakipasha leo kwenye Mazoezi ya Timu hiyo inayoongozwa na Meneja Van Gaal.Van Gaal na Doctor Jos Van D.
Kumbukumbu:
Man United ishacheza na PSV mara 5 tangu wakutane kwa mara ya kwanza 1984 walipokutana kwenye UEFA CUP na Man United kushinda 1-0 Uwanjani Old Trafford na kuibwaga PSV Jumla ya Bao 1-0 kwa Mechi 2 na kisha kucheza kwenye Kundi la UCL Msimu wa 2000/01 ambapo PSV wlishinda 3-1 kwao lakini Old Trafford Man United iliitwanga PSV Bao 3 kwa Bao za Teddy Sheringham, Paul Scholes na Dwight Yorke.
Hivyo katika mara mbili walizocheza Old Trafford Man United walishinda Mechi zote 2.

Mtu hatari:
Kwa PSV ni Luuk de Jong ambae ndie anaoongoza kufunga Mabao kwa Timu yake na pia Ligi ya Uholanzi, Eredivisie, Msimu huu akiwa na Bao 11 lakini kwenye UCL Msimu huu amefunga Bao 1 dhidi ya Wolfsburg.
Wayne Rooney

DepayBlind Kipa David De Gea

No comments:

Post a Comment