Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 14, 2017

MAYANGA AKABIDHI PROGRAMU YA MIEZI SITA TFF



KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amekabidhi programu ya miezi sita kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Akizungumza na wandishi wa habari jana Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema katika program hiyo Mayanga amependekeza mechi za kirafiki za kimataifa kabla ya mechi za ushindani.
“Mechi ambazo amependekeza ni za kwa mujibu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ambako zitachezwa kati ya Machi 21 na 29, mwaka huu,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema TFF inaratibu michezo ya Taifa Stars dhidi ya wapinzani wake za kuwania kufuzu CHAN ambazo zitafanyika Kenya mwakani.
Aprili, 20-22, 2017 kutakuwa na mechi za kufuzu kwa michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani (CHAN) ambako Taifa Stars itacheza na Rwanda katika hatua za awali.
Kwa mujibu wa ratiba, Juni 6-13, mwaka huu kutakuwa na mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Lesotho katika mchezo utakaofanyika hapa Tanzania.
 Kwenye AFCON Tanzania iko kundi “L” ambalo wapinzani wake wako Lesotho watakaoanza kucheza nao hapa nyumbani kabla ya huko mbele kucheza na Uganda na Carpe Verde, fainali za AFCON zinatarajiwa kufanyika Cameroon, mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment