Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 14, 2017

MALINZI AIPONGEZA LIPULIRAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameupongeza uongozi wa Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema katika barua hiyo ambayo alimwandikia Katibu Mkuu wa Lipuli Rais Malinzi alisema mkoa wa Iringa umepata timu ya Ligi Kuu baada ya miaka 17.
“Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabu yako, benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.
 “Bila shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali kuhakikisha mnafika hapa mlipo,” ilisema barua hiyo na kuongeza: “Rai yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katika ligi.”
 Lipuli iliyokuwa kundi “A” imepanda daraja na kuzipiku timu za Kiluvya United ya Pwani, Pamba ya Mwanza, African Sports ya Tanga, Polisi Dar, Ashanti United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment