KATIKA kuhakikisha inapiga vita matumizi ya madawa ya kulevya Shirikisho
la mpira wa miguu nchini (TFF) limeandaa ziara ya mafunzo kwa timu ya Taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ili kuwaepusha na janga hilo.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Machi 4
watafanya ziara ya kutembelea Sober house ya Life and Hope iliyopo Bagamoyo
Pwani ili wachezaji hao wakajionee jinsi madawa ya kulevya yanavyaathiri.
“Unajua
wachezaji wa Serengeti boys wapo kwenye hatua ya mabadiliko ya kimwili ambayo
huleta vichocheo vingi ambavyo husababisha kujiingiza kwenye makundi na tabia
mbaya,” alisema Lucas.
Pia Lucas
alisema wachezaji hao ambao wataandamana na waandishi wa habari watawapelekea
zawadi vijana wanaotibiwa kwenye kituo hicho ili nao wajione ni sehemu ya jamii
na kuonyesha kuwa wameguswa na janga hilo pamoja na kushiriki katika jitihada
za Serikali za kuthibiti matumizi ya dawa za kulevya.
“Vijana wa Serengeti nao wanakuwa sasa,
wanatamani kujaribu vitu vingi, wanataka kuwa na wapenzi kufanya mambo
mbalimbali kwakuwa wanajiona ni wakubwa kwahiyo tutawapeleka Bagamoyo ili
wakajionee madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya” alisema Lucas.
Suala la
madawa ya kulevya ni vita ya kila mtu hivyo TFF imeunga mkono serikali kuhakikisha
vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa haijiingizi kwenye matumizi ya dawa za
kulevya
No comments:
Post a Comment