Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 16, 2017

KUZIONA YANGA NA NGAYA JUMAMOSI NI 3000KUZIONA Yanga na Ngaya de Mbe ya Comoro katika mchezo wa marudiano raundi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika ni Shilingi 3000 kwenye viti vya kawaida.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametaja viingilio vya mchezo huo ambao utachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
“Viingilio katika mchezo wetu vimeangalia hali ya uchumi wa mashabiki kwani VIP A kiingilio kitakuwa Sh 20000, VIP B Sh 10,000, VIP C ni 10,000 na kawaida ni 3000,” alisema Mkwasa
Naye kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema wanajivunia ushindi mnono walioupata ugenini, kwani ni hazina tosha kwao lakini akasema wanatambua umuhimu wa mchezo wa marudio.
“Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu na wanamichezo wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani ushindi wetu ni wa Tanzania yote,” alisema Mwambusi
Katika mchezo huo, Yanga itawakosa wachezaji wake nyota watatu, ambao ni kiungo Haruna Niyonzima anayesumbuliwa na Malaria na washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao ni majeruhi.
Katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda mabao 5-1 mchezo uliochezwa Jumapili iliyopita Moroni Comoro.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Alex Muhabi Nsulumbi akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati mwamuzi wa akiba ni Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.