Tuesday, February 14, 2017
SIMBA KUCHEZA NA AFRICAN LYON ALHAMISI KOMBE LA SHIRIKISHO
MECHI ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba na African Lyon ambao ulikuwa uchezwe Machi mosi sasa utachezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizngumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema mchezo huo wa raundi ya sita umelazimika kuchezwa mapema kutokana na timu hizo kuomba.
“Raundi ya sita ilikuwa ianze Febuari 24 lakini Simba na African Lyon zimeomba kucheza mapema na sisi baada ya kuona ratiba inaruhusu tukawakubalia,” alisema Lucas.
Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 hivyo utachezwa mchezo huo mmoja kabla ya kuendelea tena Februari 24, mwaka huu ambapo michezo minne itachezwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni lakini mchezo mmoja utakaopigwa saa 1.00 jioni.
Michezo hiyo, itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala, mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
Februari 26, timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Machi 7, mwaka huu Yanga itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment