Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 8, 2016

YANGA KUKOSA HUDUMA YA BOSSOU NA TWITE KESHO



KOCHA wa Yanga, Hans  Pluijm amesema atawakosa walinzi wake wawili tegemeo, Mbuyu Twite na Vincent Bossou katika mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting.
Ligi Kuu ya Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mechi tatu na mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Simba watakuwa wageni wa Prisons Mbeya na Azam FC wataifuata Mwadui huko Shinyanga.
Kuelekea mchezo huo, kocha Pluijm amesema kwamba anasikitika atawakosa beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Twite na beki wa Kati Bossou.
Pluijm amesema kwamba Twite atakuwa anatumikia adhabu ya kadi, wakati Bossou amerejea kwao kuichezea timu yake ya taifa, Togo katika mechi za kimataifa zinazoanza katikati ya wiki hadi mwishoni mwa wiki
“Tunachezaji na Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa lazima kushinda. Tutawakosa majeruhi Juma Abdul, Mbuyu Twitte ana kadi na Vincent Bossou amekwenda timu ya taifa ya Togo,”amesema Pluijm.

No comments:

Post a Comment