Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 9, 2016

KABAGO AACHIA WIMBO MPYA LEO

Leo mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago", ameachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha Hadmad.

Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).

Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.

Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake. 

Kaa tayari kuusubiri wimbo wa Kabago uitwao Tanzania ambao umetengenezwa kwenye studio yake iitwayo K-Records chini ya produza Sam Music.