Vituo vya Utamaduni wa China zaidi ya 20 katika nchi tofauti duniani vitafanya maonyesho ya utamaduni wa nchi hiyo pamoja na kuenzi wasanii waliohamasisha jamii ya wachina kuenzi tamaduni zao.
Mshauri wa Ubalozi wa Watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania, Gao Wei amesema kwa hapa nchini maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Novemba 12 hadi 24, 2016 katika kituo cha utamaduni wa China kilichopo Upanga, jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tunafanya maonyesho na kumbukumbu ya mwandishi wa tamthilia za China William Shakespeare na msaidizi wake Tang Xianzu, kutokana na mchango wao katika ulimwengu wa Tamthiliya. Kumbukumbu hii itafanyika katika vituo vya kitamaduni za China vipatavyo 26 katika nchi tofautitofauti,” amesema na kuongeza.
“Maonyeshi hayo pia yanafanishwa na maisha na kazi za wasanii hao ambao walihamasisha jamii ya China kudumu na kuenzi tamaduni zao.”
Amesema maonyesho hayo yataambatana na burudani ya muziki wa asili ya China na mashairi.
“Maonyesho hayo pia yatawezesha wageni kuelewa tofauti ya tamaduni za nchi za mashariki na magharibi,” amesema.