Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 1, 2016

KIPA DANIEL AGYEI KUMWONDOA NDUSHA MSIMBAZI



KIPA Daniel Agyei raia wa Ghana aliyetua nchini jana kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Simba ambapo imeelezwa kwa asilimia kubwa atasaini mkataba wa miaka miwili huku akikumbuka jinsi alivyofanikiwa kuwazuia Yanga kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Usajili wa kipa huyo ni matakwa ya kocha Joseph Omog ambaye aliutaka uongozi umtafutie kipa mwenye uwezo mkubwa baada ya kuchukizwa na mechi mbili za mwisho ambazo Vincent Angban alifungwa dhidi ya African Lyon na Prisons. Lyon ilishinda bao 1-0 huku Prisons wao wakishinda bao 2-1.
Awali kulikuwepo na taarifa kwamba Angban anaweza kutemwa kwenye usajili huu kutokana na makosa aliyoyafanya kwenye mechi hizo yaliyodaiwa kuwa yanafanana ingawa bado uamuzi huo haujafikiwa na kwamba Jumamosi ndipo zitajulikana mbivu na mbichi kwenye usajili wao.

Habari za ndani zinasema kuwa kiungo Mussa Ndusha anaweza kupelekwa kwa mkopo ili wapate nafasi ya kusajili wachezaji wawili wa kigeni akiwemo kiungo mkabaji baada ya Jonas Mkude kudengua kusaini mkataba mpya.

Akizungumza mara baada ya kushuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Agyei alisema kuwa anaamini ataweza kucheza Simba na anafahamu uwezo wa makipa waliopo kwenye kikosi hicho akiwemo Angban ila anaamini kocha ndiye mwenye kuchagua nani amtumie.

"Naamini nitafanya vizuri hasa kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu kufikia malengo ambayo timu imejiwekea, naamini pia kocha ndiye atachagua nani amtumie. Makipa waliopo Simba si wabaya akiwemo Angban ila mimi ni mchezaji nitafanya kadri niwezavyo.

"Nilikuja hapa nikiwa na timu yangu ya Medeama tulipocheza na Yanga niliwaona mashabiki wa Simba walitupa ushirikiano mkubwa na tukatoka sare ya bao 1-1 naamini mimi nitakuwa mgeni kwenye kikosi lakini nitafanikiwa kwani kocha atajuwa jinsi gani mimi niwe ili niendane na soka la hapa," alisema Agyei.

Agyei alidaka mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika huku viongozi wa Simba wakimpongeza kwa kudaka vizuri mechi hiyo

No comments:

Post a Comment