Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 9, 2016

SIMBA YAFUNGWA NA TANZANIA PRISONS 2-1 SOKOINE



 Simba leo imepoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya kufungwa na Tanzania Prisons mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.
Simba ilianza vyema Ligi Kuu na kucheza mechi 13 mfululizo bila kupoteza, ikishinda 11 na sare mbili na ilipoteza mechi ya kwanza baada ya kufungwa na African Lyon 1-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa leo, shujaa wa Prisons alikuwa ni mchezaji wa zamani Rhino Rangers ya Tabora, Victor Hangaya aliyefunga mabao yote mawili, na lile la Simba lilifungwa na Jamal Mnyate kutangulia
Mnyate alifunga dakika ya 43 akimalizia kwa kichwa krosi ya winga Shizza Kichuya kutoka upande wa kushoto.
Simba ikaenda kupumzika inaongoza 1-0 na dakika mbili tu baada ya kuanza kipindi cha pili Hangaya akaisawazishia Prisons akimalizia krosi ya Salum Bosco kabla ya kufunga la pili dakika ya 64 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa Mohammed Samatta.
Simba ilipambana kusaka bao la kusawazisha, lakini bahati haikuwa yao.
Kwa matokeo hayo, Simba inamaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 15, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 30 ambao kesho wanacheza mechi yao ya mwisho ya mzunguko wa kwanza na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Kikosi cha Prisons kilikuwa; Andrew Ntala, Benjamin Asukile, Salum Kimenya, Leonsi Mutalemwa, James Mwasote, Njinjai Kazungu, Jumanne Elfadhil, Lambarti Sabiyanka, Mohemmed Samatta, Victor Hangaya na Salum Bosco.
Simba SC; Vincent Agban, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude/Mussa Ndusha dk82, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Mwinyi Kazimoto/Ibrahim Hajib dk69 na Jamal Mnyate.

No comments:

Post a Comment