Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 12, 2016

HAFIDH ALLY ALAMA YA SOKA LA TANZANIA ILIYOZIMIKA GHAFLAMWAMUZI pekee wa Tanzania ambaye amewahi kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia za Vijana, Hafidh Ally amefariki dunia jana, usiku katika hospitali ya General Dodoma alikopelekwa kwa matibabu.
Hafidh Ally alichezesha fainali za Vijana U-16 zilizofanyika nchini Scotland  mwaka 1989 na alikuwa mwamuzi pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambaye amewahi kuchezesha fainali za mataifa huru ya Afrika (CAN) (kwa sasa AFCON) kwa miaka sita mfululizo

Fainali za Mataifa Huru Afrika ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili, Hafidh alichezesha ni 1984  hadi zile za mwaka 1994 ambapo  1984 ndio alikuwa bingwa Cameroon, 1986 Misri ikaibuka bingwa, 1988 akawa bing
 
waCameroon
1990 wakawa bingwa Algeria, 1992 bingwa ni Ivory Coast na 1994 akachukua ubingwa Nigeria

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa waamuzi wastafu, Lesley Liunda ambaye pia ni kamishna na mkufunzi wa CAF, alisema Tanzania imepoteza moja ya alama muhimu kwenye tasnia ya uamuzi ambayo haijawahi kufikiwa na yeyote.
"Mimi nilimkuta Hafidh kwenye uamuzi, alinipokea vizuri na alikuwa ni mtu muwazi na aliyependa kusaidia wenzake nasikitika ameondoka wakati bado mchango wake unahitajika", alisema Liunda.
Pia Liunda alisema kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hakuna mwamuzi aliyeweza kuvunja rekodi ya Hafidh Ally ya kuchezesha Mataifa Afrika kwa mfufulizo mara sita.
"Kwa Afrika unaweza kupata waamuzi ambao hawazidi watatu waliochezesha mataifa kama Hafidh kwa mfufulizo hata akina Masembe wa Uganda hawajamfikia", alisema Liunda.
Liunda ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi wa FIFA alisema amewahi kuchezesha na Hafidh mechi za Simba na Yanga na kwenye Ligi ya Muungano na kudai kuchezesha naye unafurahia.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Selestine Mwesigwa alisema shirikisho limepokea kwa masikitiko kifo chake kwani TFF wamepoteza mtu muhimu kwenye soka la Tanzania
 Jina la Hafidh ni linabeba dhana zima ya waamuzi Tanzania na Afrika kwani alikuwa mkufunzi na kamishina ambaye anatambuliwa na CAF na FIFA hivyo kuondoka kwake ni pengo kwetu TFF kwani tumepoteza mtu muhimu", alisema Mwesigwa .
Hafidh pia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM),
Pamoja na wasifu huo Hafidh alikuwa mpenzi na mwanachama wa klabu ya Yanga na juzi alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Bungeni Dodoma chini ya mwenyekiti Venance Mwamoto, na Makamu Ridhiwani Kikwete.
Hafidh alizaliwa Oktoba 30, mwaka 1953 visiwani Zanzibar na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.