Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 9, 2016

MATANDIKA NA CHACHA WA TFF WAPANDISHWA KIZIMBANI LEOJuma Matandika na Martine Chache, leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh 25 milioni kwa kwa klabu ya Geita Gold Sport ili kusaidia kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu wakati kwenye ofisi za Shirikisho hilo zilizopo Karume, jijini Dar es Salaam. Geita Gold kwasasa imeshushwa daraja hadi ligi ya Wilaya baada ya kutosajili kwa ajili ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa madai kuwa rufaa yao haijasikilizwa.

Baada ya kuwepo tuhuma hizo, TFF walimsimamisha Matandika huku Chacha akijiuzulu nafasi yake wakati tayari Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) ikianza uchunguzi wake mara moja.

Kesi hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi ilisimamiwa na wakili Leonard Swai aliyeiwakilisha TAKUKURU huku upande wa serikali akisimama wakili Odesa Horombe na upande wa watuhumiwa walitetewa na wakili Claudia Nestory.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kuomba rushwa kwa viongozi wa Geita Gold Sport, Salum Kulunge na Costantine Molandi ili kuishawishi TFF  ipande daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza(FDL) hadi VPL.

Watuhumiwa walisomewa mashitaka hayo na wote walikana  ambapo kwsi hiyo imetajwa kusomwa tena Novemba 30, Matandika na Chacha wameachiwa kwa dhamana baada ya kila mmoja kulipa Sh 5 milioni.

Hivi karibuni TAKUKURU ilisema kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo umekamilika na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani. Tuhuma hizo pia zinahusisha upangaji wa matokeo kwa timu ya Polisi Tabora ambayo imeshushwa daraja hadi ligi ya wilaya pamoja na Geita.

Tabora nao waligomea kushiriki ligi ya FDL wakitaka kwanza rufaa yao isikilizwe kwa madai kuwa hawakutendewa haki na waliohusika kwenye mpango wa upangaji matokeo ni vigogo wa TFF