Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 22, 2016

MKUTANO WA SIMBA RUKSA LAKINI.........................SERIKALI imetoa baraka zake katika Mkutano mkuu wa dharura wa klabu ya Simba wa mabadiliko ya Katiba uliopangwa kufanyika Disemba 11 ikiwa utafuata taratibu kwa mujibu wa katiba yao.

Uongozi wa Simba juzi ulitangaza Mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ambayo kwa kauli moja yatapitisha suala la uendeshwaji kwa mfumo wa hisa ambapo Mohamed Dewji 'MO' amepanga kununua hisa za asilimia 51.

Katibu mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amesema endapo mkutano huo utafuata taratibu zote kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo serikali haitakuwa na pingamizi lolote.

Kiganja alisema kama hakuna malalamiko kutoka kwa wanachama wao na muda ni mrefu kabla ya mkutano kufanyika utaratibu umefuatwa basi wao wanaubariki wala hawana pingamizi.

"Serikali ipo kwa ajili ya kuongoza michezo yote nchini na kujipanga kwa kila hali kuhakikisha migogoro isiyo ya lazima inaepukwa hususani klabu za Simba na Yanga ambazo zina mashabiki wengi" alisema Kiganja.

Hivi karibuni Kiganja alipiga marufuku michakato yote ya kiuendeshaji kwa klabu hizo kongwe nchini hadi utaratibu utakapo fuatwa kwa mujibu wa katiba zao