Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 22, 2016

KIGANJA AITAKA TFF KUWEKA MKATABA NA MAKOCHA





KATIBU mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amefunga kozi ya awali ya makocha wanawake iliyoendeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Karibu Tanzania Association kwa kushirikiana na TFF
Kozi hiyo ya siku 10 ilishirikisha washiriki 27 wakiwa ni walimu toka vyuo mbalimbali vya maendeleo ya jamii na iliendeshwa na Mkufunzi wa CAF,  Wilfred Kidao.

Kiganja amelitaka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuwabana wahitimu hao kwenda kufundisha soka katika maeneo yao na sio kufungia vyeti ndani kwani elimu waliyoipata inatakiwa kuinua soka la wanawake nchini.

"Lazima TFF muweke utaratibu ambao utawabana wahitimu  wanaopata mafunzo ya kozi mbalimbali kuhakikisha wanatumia elimu wanayoipata kwa manufaa ya jamii inayowazunguka la sivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu," alisema Kiganja.
Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Katharina Rangnitt ambaye alikuwa mgeni mwaliko aliipongeza TFF kwa kutoa kozi hiyo kwa wanawake kutokana na kuthamini mchango wao ambao umekuwa ukipanda kwa kasi.

Naye Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa alisema kwa sasa timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' imekuwa ikiitangaza vizuri Tanzania barani Afrika ambapo mwaka jana ilikuwa miongoni mwa timu nane bora licha ya kushindwa kufuzu fainali za AFCON.

"Twiga Stars sasa inaogopwa Afrika na jitihada hizi tunazifanya ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri Kimataifa" alisema Mwesigwa.

No comments:

Post a Comment