Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 22, 2016

JKT QUEENS YAIADHIBU FAIR PLAY YA TANGA MABAO 12-2TIMU ya Soka ya wanawake, JKT Queens imefunga timu ya Viva ya Tanga mabao 12-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuuya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam juzi.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa upande mmoja ulihudia JKT Queens wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 6-0 na kipindi cha pili walifunga mabao sita mengine na Viva wakafunga mabao mawili.
Shujaa wa mchezo huo alikuwani mshambuliaji wa JKT Queens, Fatuma Swalehe ambaye alifunga mabao sita peke yake, akifuatiwa na Asha Rashid 'Mwalala na Zena Rashid ambao kila mmoja alifunga mabao mawili
Karamu ya mabao ilihitimishwa na Marry Masatu na Anna Hebron ambao kila mmoja alitupia nyavuni bao moja moja.
Mabao ya Viva yalifungwa na Aisha Shaban kwa njia ya penalti baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa faulo na beki wa JKT Queens, Happy Mwaipaja na lingine likafungwa na Mgeni Ramadhan.
Akizungumza baada ya mchezo, kocha wa JKT Queens, Robert Ngoliga alisema dhamira yao ni kuchukua ubingwa na ndio maana wachezaji wake wanajitahidi kuufunga mabao mengi iwezekanavyo.
"Dhamira yetu ni ubingwa na ndio maana tumefanya usajili wa uhakika na kila mechi tunahesabu kama ni fainali kwetu," alisema Ngoliga.
Timu ya JKT Queens inaundwa na wachezaji ambao asilimia kubwa wanacheza timu ya Taifa ya wanawake 'Twaiga Stars'