Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 15, 2016

KTA YAANZA KUTEKELEZA PROGRAM ZA SOKA LA WANAWAKE


Mkurugenzi wa Maendeleo wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Association, (KTA), Mia Mjengwa (katikati) akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kozi ya awali ya ukocha inayoendeshwa na KTA kwa kushirikiana na TFF kwa ajili program ya la wanawake kwenye vyuo vya maendeleo ya jamii nchini. Kulia ni mjumbe wa KTA Consolatha Luhende na kushoto ni Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas. (Picha na Rahel Pallangyo)


SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Association (KTA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) linaendesha kozi ya awali ukocha wasichana na wanawake.
Akizungumza na wandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Maendeleo wa KTA, Mia Mjengwa alisema kozi hiyo inashirikisha makocha 25 toka kwenye vyuo vya maendeleo ya jamii mbalimbali vilivyopo hapa nchini.
“Tumeanzisha program hii ili kuwapa fursa zaidi watoto wa kike na wanawake kujifunza soka kwenye jamii zao na tutakuwa tunatumia vuo vya maendeleo ya jamii kufundisha”, alisema Mia.
Pia Mia alisema kuwa kwa kushirikisha vyuo vya maendeleo ya jamii wanaamini kuwa jamii inapata fursa ya kufundishwa kwa karibu kwani vyuo hivyo vinafanya kazi karibu na jamii.
Mia alisema program hii ndio inaanza kwa kuwafundisha makocha na pia itakuja awamu nyingine kwa ajili ya kuwafundisha waamuzi.
Kozi hiyo ya siku 10 inafundishwa na mkufunzi wa CAF, Wilfred Kidao.