Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 15, 2016

FIFA KUMWAGA PESA TFFSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kuanzia mwakani litapata ruzuku ya kiasi cha dola 500,000 sawa na Sh bilioni 1 kwa ajili ya maendeleo ya soka la wanawake na vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema awali walikuwa wakipata dola 250,000 kutoka Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), lakini kuanzia mwakani dau limepanda mara mbili.
TFF kuanzia Julai mwakani tutakuwa tukipata ruzuku ya dola 500,000 ikiwa mara mbili ya zile za awali kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana na wanawake na hii imetokana na maendeleo mazuri ya soka hilo hapa nchini, alisema Lucas.
Pia Lucas alisema kutokana na timu za vijana na wanawake kupata ruzuku hiyo ndio maana timu hizo zinasafiri kucheza mashindano mbalimbali.
Mtakumbuka Kilimanjaro Queens walikwenda kwenye mashindano ya Chalenji ghafla kwa sababu ya ruzuku hiyo na tunashukuru walifanya vizuri, jambo ambalo limesaidia Tanzania kujulikana kwenye medani ya kimataifa kwa ajili ya soka la wanawake na vijana, alisema Lucas.
Lucas alisema Twiga Stars imerudi jana usiku kutoka Cameroon, ambapo ilicheza michezo miwili ya kirafiki huku ikishinda mmoja na kupoteza mwingine.
Hatahivyo, wadau wa soka wamekuwa na wasiwasi kama kweli fedha hizo zilikuwa zikitumika vizuri, kwani timu za wanawake mara kadhaa zilikuwa zikilalamikia posho na mambo mengine.