Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 15, 2016

UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA IRINGA KURUDIWA


Mwenyekiti wa kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Dk. Mutabazi Rogazia, akitoa maamuzi kuhusu rufaa ya kupinga uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Iringa kwa wandishi wa habari. Kulia ni Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas. (Picha na Rahel Pallangyo)


KAMATI ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania, imefuta uchaguzi wa Chama cha Soka mkoa wa Iringa (IRFA) na kuagiza mchakato kuanza upya ndani ya siku 14.
Akizungumza na wandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Dk. Mutabazi Rogazia, alisema kamati yake ambayo ilikutana Novemba 13 ilipokea rufaa mbili toka mkoa wa Iringa zikipinga uhalali wa uchaguzi huo.
“Mchakato wa uchaguzi ulikuwa batili  hivyo utangazwe upya pamoja na taratibu za uchukuaji fomu ziane upya hata wale ambao hawakuchukua fomu wanaruhusiwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi na mchakato huu utaanza Novemba 20”, alisema Dk Rogazia
Pia Dk. Rogazia aliagiza Shirikisho la soka (TFF) lipeleke wajumbe wengine kusimamia uchaguzi  na zoezi zima la mchakato kwani uwepo wa Juma Lalika kwenye kamati ya uchaguzi kunabatilisha zoezi zima kwani kwa vile ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF na pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya mkoa huo
Dk. Rogazia alisema kamati yake ilipokea rufaa ya Festo Mkemwa ikipinga Kamati ya Soka ya Mkoa wa Iringa, kumpitisha Syprian Kuyava ambaye ni Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti mkoa huo.
Na rufaa nyingine ilikatwa na Ramadhan Mahano, akipinga kamati ya mkoa kumpitisha Abdulsufiani Omar kuwa mgombea wa nafasi ya uchaguzi wa TFF.

Dk. Rogazia alisema wakata rufaa wote walipinga maamuzi ya kamati kumpitisha wagombea hao kwa sababu hawakuwa na uzoefu wa kuongoza wa miaka mitano pia mwenyekiti aliyemaliza muda wake hakuwahi kuitisha kikao hata kimoja katika vile viakao ambavyo vipo kisheria.
Mjibu rufaa Kuyava alijitetea na kupinga kwani aliwahi kuwa kiongozi wa Hazina sports club  ya Dar es Salaam mwaka 2008  na alichaguliwa tena 2011  hadi sasa lakini hakuwahi kuleta uthibitisho kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wa kuwa aliwahi kuongoza timu  hiyo hadi mchakato wa uchaguzi unamalizika.
Pia Dk. Rogazia alisema swala la kuwepo kwa vikao lilitibitishwa na Juma Lalika ambaye ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, huku pia akiwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya mkoa huo na wakata rufaa wakishindwa kuthibitisha rufani zao.
Uchaguzi huo umebatilishwa na kamati ya rufaa kwasababu Juma Lalika hakusatahili kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF na ya mkoa hapohapo tena anakuwa mjumbe wa kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Endapo wakati wa zoezi la uchaguzi kutatokea kwa zoezi la upigaji kura na matokeo yake ama kwa moja kwa moja au kwa taswira yake jambo hilo litachukuliwa kwa uzito wake na kuagiza kamati zote za uchaguzi za TFF kuepuka kufanya mambo ambayo yapo kinyume na katiba.