Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 25, 2016

KABETE JUKWAANI KESHO MISS AFRIKA



MWAKILISHI wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika 2016,  Julitha Kabete, kesho atapanda jukwaani moja na washiriki wenzake 18 kuwania taji la mrembo wa michuano hiyo linalofanyika nchini Nigeria.
Mashindano haya yatakayofanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River, Calabar , mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajipatia kitita cha dola za Kimarekani 25,000, sawa na Sh.milioni 52 ya Tanzania  pamoja na gari jipya.
Mshindi  wa pili katika shindano hilo atapata kitita cha dola ya Kimarekani 15,000  sawa na Sh.milioni 33 za Kitanzania na wa tatu  dola 10,000  sawa na Sh.milioni 22.
Akizungumza na Gazeti hili, mshiriki huyo alisema kikubwa anaomba Watanzania wamuombea dua haweze kushinda taji hilo.
Kabete alisema kuna upinzani mkali, lakini nae kwa upande wake anajiamini anauwezo mkubwa wa kufanya vizuri na kubeba taji la shindano hilo.
"Nina nafasi ya kufanya vizuri, kikubwa naomba dua zetu Watanzania wenzangu, niweze kufaya vizuri na kubeba taji,"alisema Kabete.

Mrembo huo ameenda kushiriki shindano hilo alikiwa chini ya kampuni ya Millen Magese  Group (MMG), inayomilikiwa na Happiness 'Millen' Magese, anayefanya shughuli zake za mitindo nchini Marekani.